Breadcrumbs

PF Publications

Bajeti ya Serikali ya Mwaka 2011- 2012

Bajeti ya Mwananchi ni bajeti iliyorahisishwa na ambayo imewekwa katika muundo unaomfanya mwananchi wa kawaida aweze kuelewa
mambo muhimu ambayo Serikali imeyapanga katika mwaka wa fedha. Bajeti hii ya mwananchi inalenga kufanya taarifa za kifedha zieleweke kwa urahisi na mwananchi wa kawaida na kuwapa wananchi fursa ya kuelewa mipango ya Serikali na mchakato wa kutekeleza bajeti hiyo. Bajeti inataja kwa ufupi wapi Serikali itapata fedha na jinsi ilivyojipanga kutumia fedha hizo.Tafadhali angalia kiambatanisho hapo chini kwa kusoma zaidi.

Kufungwa kwa ofisi ya PF Sekretariati

Tunapenda kuwataarifu kuwa ofisi ya Sekretarieti ya Policy Forum itafungwa  kwa likizo ya Krismasi na Mwaka Mpya kuanzia Desemba 20, 2011 Jumanne hadi Ijumaa  Januari 6, 2012.

Ofisi itafunguliwa na kuanza tena shughuli zake za mara kwa mara tarehe Jumatatu Januari 9, 2012.

Mgawanyo wa bajeti ya Sekta ya Kilimo: Je, nini hatma ya wakulima wadogo Tanzania?

Kama sekta ya kilimoTanzania itawekezwa ipasavyo ina mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini. Kwa mujibu wa taarifa ya bajeti 2011/12 iliyotolewa na Waziri mwenye dhamana ya kilimo, kwa sasa sekta hii ina ajiri asilimia 77.5 ya watanzania na kuchangia asilimia 95 ya chakula kinachotumika nchini. Sekta ya kilimo pia inaonekana kukua kwa asilimia 4.2 tangu mwaka 2010 kutoka asilimia 3.2 ya mwaka uliotangulia.

Kwa nini afya siyo kipaumbele katika bajeti ya taifa 2011/12

Mchakato wa bajeti ya mwaka unatoa fursa ya kutathmini kama taarifa kwa umma kuhusu vipaumbele vya serikali vinafuatwa. Kwa mfano, katika miaka ya hivi karibuni serikali imeonyesha nia ya kutaka kupata thamani halisi ya fedha kadri inavyotoa bajeti yake ili kuweza kukabiliana na matumizi yasiyo ya lazima. Uchambuzi huu wa bajeti ya sekta ya afya 2011/12 kwa ufupi unatoa malengo maalumu yanayo tathmini thamani ya fedha. Uchambuzi unapima jinsi rasilimali zilizopo zimeweza kugawanywa na kama mgawanyo huo utaweza kuleta mabadiliko katika sekta ya afya.

Ijue Sheria Mpya ya Madini Namba 14 ya 2010

Sheria hii mpya ya madini imetungwa baada ya mchakato mrefu uliotanguliwa na Kamati na tume mbalimbali zilizoundwa pamoja na msukumo mkubwa kutoka asasi za kiraia na kuhitimishwa na Tume iliyoongozwa na Jaji Mstaafu Mark Bomani iliyoundwa mwaka 2007. Sheria hii inaweka utaratibu wa kisheria katika kutekeleza sera mpya ya madini ya mwaka 2009. Sheria hii ya madini namba 14 ya mwaka 2010 ilipitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 23 Aprili 2010 na kusainiwa na Rais tarehe 20 Mei, 2010.

Ushawishi Bungeni Katika Tasnia ya Madini

Mwongozo huu umetolewa na Policy Forum katika jitihada zake za kurekodi yale yaliyojiri waliposhirikiana na wabunge katika kuchangia sheria mpya ya madini Tanzania, na kuboresha uwezo wa asasi za kiraia na vyombo vya habari katika kusimamia utendaji wa serikali kwenye sekta ya uziduaji (mafuta, gesi asilia na madini). Programu hii ilifanyika kwa ushirikiano na taasisi ya Revenue Watch. Kusoma zaidi tafadhali angalia viambatanisho hapo chini

Utawala wa Kidemokrasia katika Jamii (5th Edition, 2011)


Mwananchi ana wajibu na majukumu yake kuhakikisha kuwa Kiongozi aliyemchagua au kuteuliwa anatimiza wajibu wake ipasavyo katika viwango vinavyokubalika katika eneo la kijiji/mtaa kulingana na mipango na makubaliano ya vikao vya kisheria vya kijiji na mtaa. Kila mwananchi ana wajibu wa kupinga na kukataa kila aina ya uovu katika jamii ikiwemo rushwa, uonevu, wizi, ubadhirifu wa mali za umma na ya watu binafsi. Kwa maelezo zaidi tafadhali angalia viambatanisho hapo chini.

Mwongozo wa Katiba kwa Raia

Kitabu cha Mwongozo wa Katiba kwa Raia” ni chapisho ambalo linatoa mchango katika mchakato mzima wa kupata Katiba mpya hapa nchini kwetu.
Madhumuni ya kitabu hiki ni kujenga na kuongeza uelewa wa watanzania juu ya Katiba, historia yake na mchakato wa uandikaji
wa Katiba hapa nchini na duniani. Dhumuni la pili ni kuwatoa hofu watanzania kuwa uandikaji wa Katiba si suala la wanasheria tu bali

TAFSIRI RAHISI YA MALENGO YA MKUKUTA II

2.0 USULI
MKUKUTA ni nini? Ni kifupisho cha maneno ya Kiswahili yenye maana ya Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini Tanzania. Kuendelea kusoma bofya hapa

Utawala wa Kidemokrasia katika Jamii

Mwananchi ana wajibu na majukumu yake kuhakikisha kuwa Kiongozi aliyemchagua au kuteuliwa anatimiza wajibu wake ipasavyo katika viwango vinavyokubalika katika eneo la kijiji/mtaa kulingana na mipango na makubaliano ya vikao vya kisheria vya kijiji na mtaa. Kwa taarifa kamili tafadhali bofya hapa.