Majadiliano juu ya nafasi ya Mazingira na Maliasili katika katiba mpya ya Tanzania
Tanzania inaelekea kipindi cha marekebisho ya kihistoria ya katiba yake, mchakato umeshika kasi kubwa baada ya uchaguzi mkuu wa 2010. mchakato wa marekebisho haya yanayoendelea kwa kiasi kikubwa umeweka mbele masuala ya kupunguza nguvu za rais, haja ya kubadili Tume ya Taifa ya Uchaguzi, suala la haja kwa wagombea binafsi, na uchaguzi huru na wa haki. Kipaombele kidogo sana, hata hivyo, kimewekwa kwa upande wa kuingiza masuala ya mazingira na maliasili katika katiba. Kama wote tunavyojua, haya ni ya msingi kwa ustawi wa Watanzania na jumuiya ya kimataifa kwa ujumla.
Kwa maana hii, mjadala wa kitaifa ni muhimu ili kuhakikisha kwamba wadau wa mazingira na maliasili wa ndani na nje nchi wanatoa maoni yahusianayo na mchakato wa marekebisho wa katiba unaoendelea.Bila hivi, mchakato unaoendelea wa mageuzi ya katiba unauwezekano wa kuhusisha masuala ya siasa zaidi.
Hivyo, Idara ya Jiografia katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam inaandaa warsha hii kuanzisha mjadala juu ya nafasi ya mazingira na maliasili katika katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. washiriki wengine wakubwa ni, Lawyers Environmental Action Team (LEAT), Policy Forum, Jukwaa la Katiba, na Tanzania Natural Resource Forum (TNRF).
Mada tatu tofauti zitawasilishwa kwa kuanzisha mjadala, ambao unataka kutoa mchango wao katika mchakato wa marekebisho ya Katiba ya Tanzania.
washiriki wa warsha hii kutoka taasisi za serikali, mashirika yasiyo ya kiserikali, mashirika ya kiraia, taasisi za kitaaluma na umma kwa ujumla.
Kwa maelezo zaidi wasiliana na Alex Ruchyahinduru kupitia policy2@policyforum.or.tz