Semina ya Ukwepaji Haramu wa Mitaji Iliyofanyika Mwanza

 

Alex Ruchyahinduru, Meneja wa Mawasiliano na Uchechemuzi wa Policy Forum akiwasilisha mada

Mnamo tarehe 29 Novemba 2011 kulikuwa na semina ambayo iliyoandaliwa na Forum Syd, Mwanza Policy Initiative na Policy Forum ya  ukwepaji haramu wa mitaji katika nchi maskini iliyofanyika Victoria Palace Hotel, Mwanza.

Dhumuni la semina hiyo ni kuonyesha kiwango kikubwa cha pesa kinachopotea katika ukwepaji huu haramu wa mitaji katika nchi maskini kwa mwaka ambacho ni mara kumi zaidi kuliko misaada kutoka nje ya nchi na inapelekea upotevu mkubwa wa mapato ya umma. Ukwepaji haramu wa mitaji ukitokomezwa mapato ya Tanzania yangetosha kufikia malengo ya maendeleo milenia nchini. semina iliongelea matokeo ya ukwepaji haramu wa mitaji na nafasi ya asasi za kiraia katika kutokomeza ukwepaji haru wa mitaji.Ilionyesha kwanini ukwepaji huu haramu ni kitu kikubwa na muhimu kwa mashirika ya maendeleo ambayo yanafanya kazi ya haki na demokrasia katika njia moja au nyingine.

Waongeaji wa simina hiyo walikuwa ni Kristina Froberg, Afisa wa Uchechemuzi wa Forum Syd aliyezungumzia ukwepaji haramu wa mitaji kimataifa, Jimmy Luhende kutoka MPI, alizungumzia katika kanda ya ziwa na Alex Modest Ruchyahinduru- Meneja wa Mawasiliano na Uchechemuzi wa Policy Forum, alizungumzia katika nchi ya Tanzania.

Picha Nyingine:

Picha ya Washirika katika semina

Kristina Froberg Akiwasilisha Mada

Jimmy Luhende akiwasilisha mada