OWM-TAMISEMI Kufanya Mashauriano na AZAKI kuhusiana na Chaguzi za Serikali za Mitaa 2009.

Wakati Wizara ikiwa inasimamia Chaguzi za Serikali za Mitaa, Ofisi ya Waziri Mkuu- Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(OWM-TAMISEMI) imevialika vyama 9 vya kiraia Oktoba 10 2008 katika kikao Mjini Dodoma ili kushauriana na kupata michango yao kuhusiana na chaguzi za Serikali za Mitaa oktoba 2009. Kikao kama hiki pia kilifanyika kati ya Wizara na Vyama vya Siasa mnamo tarehe 16-17 of Septemba 2008.

Kama mmoja wa waalikwa, Policy Forum kuputia kikundi kazi chake cha Serikali za Mitaa (LGWG) pia wataudhulia kikao hicho cha mashauriano. Tokea mwaka jana(2007) kikundi kazi cha Serikali za Mitaaa kimekuwa kikishauri Serikali,  kupitia vikao vyake vya mashauriano na OWM-TAMISEMI, kuchukua hatua muafaka ili chaguzi za Serikali za Mitaa zisimamiwe na Tume ya Taifa ya Uchaguzito kama ilivyo kwa chaguzi za Uraisi na Wabunge. Hii ikiwa ni pamoja na swala la kurudisha chaguzi za Madiwani katika chaguzi za Serikali za Mitaa, yatakuwa mojawapo ya mambo ambayo yatawasilishwa na kikundi kazi kwa kushirikiana na AZAKI zingine katika kikao hicho cha mashauriano.

 Tutawaletea yaliyo jiri zaidi katika kikao hicho kwenye tovuti hii.