Kuboresha Uwajibikaji wa Serikali za Mitaa: Fursa Ziko Waapi

Ni maslahi ya nani yanayozingatiwa wakati wa kupanga na kufanya maamuzi mengine? Kuna mikakati gani ya kuiwajibisha serikali katika utendaji wake? Tofauti nyingine ya muhimu ni kati ya uwajibikaji kwa jamii ama kwa ngazi za juu serikalini na wahisani. Kipeperushi hiki kinatoa muhtasari wa mchakato wa upangaji katika serikali za mitaa, na kinatoa mawazo juu ya namna Asasi za Kiraia na nyingine zinavyoweza kuongeza uwajibikaji wa serikali za mitaa kwa jamii.

Bajeti ya SM: Pesa za SM zinatoka wapi?
Sehemu kubwa ya fedha za Serikali za Mitaa (SM) hutoka Serikali kuu: Ruzuku za Uendeshaji, Mifuko ya Sekta Maalumu, Ruzuku ya Maendeleo ya SM (LGCDG) na ruzuku maalum za maendeleo. Kiasi kingine kidogo hutokana na mapato ya kodi za ndani. Chati hii hapa chini inaelezea uhamishaji wa fedha na maelezo ya kina ya viwango vya bajeti kwa mwaka 2008-09.

Endelea

AttachmentSize
Kuboresha 2.pdf2.93 MB