Our employees
- Employee namePositionAfisa Programu- Uwezo na Uwezeshaji
Richard Angelo ni muhitimu wa chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambapo alimaliza shahada yake ya Sanaa na Jamii mwaka 2006, Kabla ya kujiunga Policy Forum alifanya kazi shirika la HakiElimu kama mkufunzi na mshauri katika kitengo cha mawasiliano. Alijiunga na Policy Forum mwaka 2008 kama Msaidizi wa Programu-Habari, Mawasiliano na Uchechemuaji na sasa hivi ni Meneja wa Uwezo na Uwezeshaji. Anapendelea kuandika na mambo ya maendeleo ya jamii.
- Employee namePositionAfisa Programu-Sera na Uchambuzi wa Bajeti
Christina Genda alimaliza shahada yake ya elimu ya usaikolojia katika chuo kikuu cha Dar es Salaam mwaka 2008 na alijiunga na The Foundation for Civil Society kama mkufunzi. Christina alijiunga na Policy Forum mwaka 2009 kama Msaidizi wa Programu-Sera na Uchambuzi wa Bajeti na sasa ni Afisa Programu-Sera na Uchambuzi wa Sera, Anapendelea sana kujihusisha na mambo ya maendeleo ya jamii.
- Employee namePositionMeneja-Sera na Uchambuzi wa Bajeti
Johnson Kaijage alijiunga na Mtandao wa Policy Forum mwaka 2010 kama Meneja-Sera na Uchambuzi wa Bajeti. Anahusika na kuratibu uchambuzi wa bajeti na shughuli zote za kikundi kazi cha bajeti. Kabla ya kujiunga na Policy Forum alifanya kazi serikalini kama mwanasheria na Afisa Programu. Ni muhitimu wa Makerere University (LL. B) na Institute of Finance Management (MBA-IB). Anapendelea marekebisho katika mchakato wa bajeti.
- Employee namePositionMratibu
Semkae Kilonzo alianza kazi Policy Forum mwaka 2007 kama Meneja anayehusika na habari, Mawasiliano na Uchechemuaji katika ofisi za mtandao wa sekretarieti, Sehemu ya matamanio yake ni kuona taarifa za uchambuzi wa sera zina sambazwa ipasavyo kwa watengeneza sera,asasi za kiraia na raia wote kwa ujumla. Na kwa sasa ni Mratibu, anayeongoza sekretarieti. Semkae ana shahada ya uzamili katika uandishi wa habari na masomo ya habari katita chuo cha Cardiff, Uingereza na kupata mafunzo ya habari Dublin Ireland na Shule ya Uandishi wa Habari Tanzania, Anapendelea kuhimiza watu wote kujihusisha katika shughuli za zote kutengeneza sera.
- Employee namePositionDereva
Rashid Kulewa alijiunga sekretarieti ya Policy Forum mwaka 2010, Alimaliza kozi yake ya komputa ICL Training Centre na amefanya kazi na mashirika tofauti kama FHI amabapo alikuwa kama dereva na Axios Foundation kama dereva na msaidizi wa afisa mgavi. Rashid anapendelea kuona watu wa Tanzania wanafaidika na mali asili za nchi yao.
- Employee namePositionAfisa Utawala na Fedha
Gibons Mwabukusi alijiunga Policy Forum mwaka 2010 kama Afisa Utawala na Fedha.Kabla ya kujiunga na Policy Forum alifanya kazi na mashirika tofauti yasiyo ya kiserikali katika mambo ya utawala na fedha. Ana stashahada ya juu ya uhasibu aliyopata kutoka Taasisi ya Uhasibu Tanzania. Matamanio yake ni kuona Policy Forum ikiwa kipao mbele katika kuhamasisha utawala bora na uwajibikaji.
- Employee namePositionMsaidizi wa Ofisi
Amani Ndoyella alijiunga na Sekretarieti ya Policy Forum mwaka 2004 baada ya kumaliza masomo yake ya National Board for Materials Management (NBMM) Certificate. Na sasa hivi anahusika na utaratibu wa ugavi,orodha/hesabu za ofisi na kukatalogi taarifa muhimu kwa wanachama wa Policy Forum. Amani anapendelea kuona mali asili za Tanzania zinatumika ipasavyo ili kuleta maisha bora kwa watu wote wa Tanzania.
- Employee namePositionMsaidizi wa Programu-Mawasiliano na Uchechemuaji
Nuru Ngailo ameanza kazi Policy Forum mwaka 2011 kama Msaidizi wa Programu-Mawasiliani na Uchechemuaji, Ana shahada ya Sheria ambayo ameipata chuo cha Kishirikishi cha Tumaini, Iringa ambapo alihitimu mwaka 2010.Matamanio yake ni kuona watu wa Tanzania wana sauti kubwa katika mchakato mzima wa kutengeneza sera.
- Employee namePositionMeneja-Habari, Mawasiliano na Uchechemuaji
Alex M. Ruchyahinduru amefanya kazi na mashirika mbalimbali ya misaada ya kibinadamu katika eneo la mawasiliano tangu mwaka 1996 na alianza kufanya kazi na shirika la Policy Forum tangu mwaka 2009 kama Meneja - Habari, Mawasiliano na Uchechemuaji. Alex anashahada ya juu ya Masiliano na Maendeleo kutoka chuo kikuu cha Gregoriana - Italy na awali, alipata mafunzo ya habari katika chuo kikuu cha Mt Augustine nchini Tanzania.
- Employee namePositionMsaidizi wa Programu-Uwezo na Uwezeshaji
Prisca Kowa ni muhitimu wa chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambapo alipata shahada yake ya Sanaa na jamii mwaka 2009. Kabla hajajiunga na sekretarieti ya Policy Forum kama Msaidizi wa Programu-Uwezo na Uwezeshaji mwaka 2011, alifanya kazi na CARE International na Aga Khan Foundation,Katika mashirika yote alijihusisha na mambo ya jamii.Prisca anapendelea kujihusisha na mambo ya uchambuzi wa sera na kazi za jamii kwa ujumla.