Dira: Policy Forum ni asasi huru yenye dhamira ya kuhusisha wananchi, asasi zisizo za kiserikali, na sekta zote zingine za jamii katika michakato ya uundwaji wa sera. Dhamira hii pia inahusisha kuwezesha hatua zote za michakato ya uundwaji wa sera zinaelimisha wananchi, zinakuza uwezo wao wa kujihusisha na zinaendeshwa kwa njia inayotoa nafasi ya uwajibikaji.

Kidokezi cha Filamu ya Kijiji cha Tambua Haki - Filamu ya Utawala bora na Uwajibikaji katika Jamii

Policy Forum kwa kushirikiana na Kanumba the Great Films wanayo furaha kuitambulisha filamu ya Kijiji cha Tambua Haki, Filamu ambayo inakusudia kuielimisha jamii mambo ya utawala bora na uwajibikaji katika jamii.

Tafadhali angalia kidokezi cha filamu hiyo.

Majadiliano juu ya nafasi ya Mazingira na Maliasili katika katiba mpya ya Tanzania

Tanzania inaelekea kipindi cha marekebisho ya kihistoria ya katiba yake, mchakato umeshika kasi kubwa baada ya uchaguzi mkuu wa 2010. mchakato wa marekebisho haya yanayoendelea kwa kiasi kikubwa umeweka mbele masuala ya kupunguza nguvu za rais, haja ya kubadili Tume ya Taifa ya Uchaguzi, suala la haja kwa wagombea binafsi, na uchaguzi huru na wa haki. Kipaombele kidogo sana, hata hivyo, kimewekwa kwa upande wa kuingiza masuala ya mazingira na maliasili katika katiba. Kama wote tunavyojua, haya ni ya msingi kwa ustawi wa Watanzania na jumuiya ya kimataifa kwa ujumla.

Semina ya Ukwepaji Haramu wa Mitaji Iliyofanyika Mwanza

 

Alex Ruchyahinduru, Meneja wa Mawasiliano na Uchechemuzi wa Policy Forum akiwasilisha mada

Mnamo tarehe 29 Novemba 2011 kulikuwa na semina ambayo iliyoandaliwa na Forum Syd, Mwanza Policy Initiative na Policy Forum ya  ukwepaji haramu wa mitaji katika nchi maskini iliyofanyika Victoria Palace Hotel, Mwanza.

RSS feed
[?]
RSS Feed
How to use RSS feed - click here for more info and help